Sera ya Kitaifa ya Ulinzi wa Jamii Nchini Kenya

Tafsiri:
en_US

Sera ya Kitaifa ya Ulinzi wa Jamii ni hatua ya ulinzi inayoongeza fursa kwa watu masikini na inakusudia kuboresha maisha yao na ustawi. Pia husaidia watu wanaopata kipato kudumisha viwango fulani vya mapato ili kuhakikisha kuwa wanaweza kupata msaada na usalama wa kijamii na kiafya.

Kifungu 43 cha Katiba ya Kenya kinasisitiza kuwa Wakenya wana haki za Uchumi, Jamii na Utamaduni. Ni haki kwa kila mtu ambaye anahitaji Serikali kutoa usalama unaofaa kwa watu wote na wategemezi wao katika wakati ambao hawana uwezo. Usalama unahusishwa na haki zingine kama vile haki ya kupata huduma za afya, hadhi na hali sahihi ya kufanya kazi.

Ni Nini Malengo ya Sera ya Kitaifa ya Ulinzi wa Jamii?

Malengo ya uhakikisho wa kijamii ni kuhakikisha kwamba Wakenya wanaishi maisha ya heshima na kufikia uwezo wao wa kibinadamu kwa kufanikisha uboreshaji wa kijamii na kifedha. Malengo haya ni:
• Kulinda Wakenya kutokana na mshtuko ambao unaweza kuwasukuma katika umasikini uliowazuia kuishi maisha yenye hadhi.
• Kusaidia familia masikini ili waweze kuhitimu kutoka kwa usaidizi wa kijamii na kuweza kujikimu kifedha.
• Kulinda watu ambao wanapata mishahara kutokana na athari za umaskini ambazo zinaweza kuwazuia kupata huduma za afya hata baada ya kustaafu.
• Kuhimiza watu maskini kuchangia katika rasilimali na mtaji wa binadamu ili kuwazuia kwenye mzunguko mbaya wa umaskini.
• Kuhimiza uhusiano miongoni mwa watu wa viwango mbali mbali ya maisha ili kuhakikisha mafanikio ya sera hii.
• Sera hii inaongozwa na kanuni kadhaa kama vile uongozi na uadilifu, utawala sahihi na usawa wa kijinsia.
• Sera hii inahakikisha mabadiliko ya maisha na ushiriki wa umma

Je Ni Nini Kanuni za Kitaifa za Ulinzi wa Jamii?

Sera hii ina aina tatu ya vitengo ambavyo ni: msaada wa kijamii, usalama wa kijamii na bima ya afya.

1. Msaada wa Kijamii

Kupitia msaada wa kijamii, serikali itatoa rasilimali zinazohitajika ili kutoa msaada kwa wakazi. Pia itabuni na kuratibu mipango na njia za maendeleo, kama bima ya afya na usalama wa kijamii. Kwa kufanya utafiti, serikali itakuwa katika nafasi ya kutambua maeneo ambayo yanahitaji uingiliaji, kama vile ushiriki wa jamii.

2. Usalama wa Kijamii

Serikali imepanga kuanzisha usalama wa kijamii ambao utahusisha wafanyakazi wote katika sekta rasmi na isiyo rasmi. Pia inakusudia kupanua huduma kwa wategemezi wa wafanyakazi hao. Licha ya hayo itaongeza ufikiaji wa kijiografia kwa huduma bora kwa kuhakikisha kwamba michango inakusanywa vizuri na kwamba kuna malipo bora ya faida kwa watu binafsi.

3. Bima ya Afya

Serikali inafanya kazi kuhakikisha kwamba Wakenya wote wanapata na mfuko wa bima ya hospitali ya kitaifa (NHIF). Bima ya afya inajumuisha huduma zote za kiafya toka utunzaji wa mama hadi virusi vya ukimwi. Serikali inaanzisha mfumo kwa watu katika sekta binafsi kuwa wanachama wa NHIF na pia kuhakikisha kwamba NHIF inajumuisha hospitali za kibinafsi. NHIF pia itaongezwa kwa mashinani ili Wakenya wote waweze kupata huduma za afya kwa bei nafuu.

Je Ni Nini Manufaa ya Sera ya Kinga ya Jamii ?

• Inasukuma maendeleo ya uchumi nchini Kenya na kuwapa Wakenya ajira yenye hadhi.
• Hupunguza tofautia kati ya Wakenya.
• Kukuza amani miongoni Wakenya.
• Kuhakikisha kwamba Wakenya wanapata huduma bora za afya kwa bei nafuu.
• Kulinda Wakenya kutokana na athari kubwa za umaskini na ukosefu wa maisha yenye heshima.
• Kuhakikisha kwamba Wakenya hawakabiliwi na njaa na mshtuko mingine ambayo inatokana na janga la umaskini.

Serikali imehakikisha ulinzi wa kijamii kwa kushirikiana na ofisi za serikali, mashirika yasiyo ya serikali, jamii na washirika wa maendeleo. Kutokana na uhaba wa ajira kwa viwango vya juu, umaskini umekithiri nchini Kenya, Sera ya Kinga ya Jamii inaweza kuwa namna nzuri ya kuwalinda Wakenya kutokana na mshtuko wa uchumi.