Unachohitajika Kujua Kuhusu Ushuru Nchini Kenya

Tafsiri:
en_US

Watu wengi hawaelewi kwa nini serikali hulazimika kuwatoza sehemu ya mapato yao. Ni kawaida kwetu sote kuwa na matamanio ya kuishi katika nchi ambayo maendeleo yatatufaidi na hata hadi vizazi vyetu vya baadaye. Hivyo basi, tuna wajibu wa kujumuishwa kugharamia huduma hizi.

Nchini Kenya, Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru (KRA) ni shirika lenye jukumu la kukusanya ushuru kwa niaba ya serikali. Mchakato wa kulipia ushuru umerahisishwa kupitia jukwaa la kidijitali; iTax.

Ili kuwa upande salama wa sheria, ni muhimu kuelewa aina tofauti za kodi zilizopo na mahitaji husika. Kwa sababu hiyo, makala haya yatazungumzia mambo yote unayohitaji kujua kuhusu ushuru nchini Kenya.

Aina za kodi Kenya

Aina za Kodi nchini Kenya

Je kuna aina ngapi za kodi? Nchini Kenya, makundi mawili mapana ya kodi ni kodi ya dhahiri na ile isiyokuwa ya moja kwa moja. Kodi ya dhahiri hurejelea sehemu ya mapato ya mtu ambayo hutozwa na serikali. Kwa upande mwingine, kodi isiyo ya moja kwa moja inalipwa wakati mtu ananunua bidhaa au kupokea huduma fulani. Makundi haya mawili ya kodi yamegawanywa zaidi ifuatavyo:

Kodi ya mapato

Wakazi wote na hata wasio wakazi nchini Kenya wanatakiwa kulipa kodi hii ya mapato.

Kampuni na watu binafsi hulipa kodi hii kwa njia ya:

Kodi ya Mashirika (Corporation Tax)

Kodi hii hulipwa na kampuni kutokana na mapato yao ya kila mwaka. Kampuni za humu nchini na za kigeni hutozwa asilimia 30 na 37.5 ya mapato yao ya kila mwaka, mtawalia.

Withholding Tax

Kodi hii hutozwa wakati wa kulipa watu wasiokuwa wafanyakazi kutokana na vyanzo vifuatavyo vya mapato:

  • Gawio
  • Faida
  • Mirahaba
  • Kodi inayopatikana kwa wakazi wasio
  • Ada ya kitaalamu au usimamizi
  • Malipo ya uzeeni
  • Asilimia ya faida (anayopewa muuza bidhaa)

Kodi ya Kulingana na Mapato (PAYE)

Hii ni kodi inayotozwa kwa kutoka watu wote walioajiriwa na waajiri huiwasilisha kwa KRA kufikia tarehe 9 ya kila mwezi. Kiasi kinachotozwa kinategemea kiwango kilichowekwa.

Kodi ya Kiawamu (Installment Tax)

Kodi hii huhusisha watu ambao, kila mwaka wao hulipa kodi ya shilingi 40,000 au zaidi.

Kodi ya Awali/Mapema (Advance Tax)

Aina hii ya kodi ya mapato hulipwa kabla ya gari la biashara au uchukuzi wa umma gari kupelekwa kwa ajili ya ukaguzi wa kila mwaka.

Ushuru wa Mapato ya Kodi (Rental Income Tax)

Hiki ni kiasi cha ushuru kwa serikali kutoka kwa watu binafsi au kampuni ambazo hukodisha mali zao. Kiasi cha kodi hulipwa kwa kutegemea kama majengo hayo ni ya matumizi ya kibiashara au makazi. Ili kurahisisha utekelezwaji wa matakwa, kuna mawakala mbalimbali wa KRA wanaosaidia kuwezesha mchakato huu. Wakala anaweza kuthibitishwa kwenye iTax.

Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)

Kodi hii kulipwa kwa bidhaa na huduma zinazosambazwa. Hutozwa kwa bidhaa zote za nje na ndani mwa nchi. Kampuni ambazo kila mwaka zina kiasi cha mapato kisichozidi Shilingi milioni 5 na zinastahili kujiandikisha kwa ajili ya VAT. Sawa na Ushuru wa Mapato ya Kodi, kuna mawakala mbalimbali wa KRA ambao husaidia katika utaratibu wa utekelezwaji wa matakwa.

Tazama video hapo chini kuhusu VAT:

 

Ushuru Wa Bidhaa (Excise Duty)

Hii ni kodi ambayo hulipwa kwa ajili ya bidhaa zinazozalishwa nchini pamoja na bidhaa zinazoagizwa kutoka nje zilizoorodheshwa kwenye Sheria ya Ushuru wa Bidhaa ya 2015.

Kodi kwa Niaba ya Mashirika (Agency Revenue)

KRA hukusanya ada hii kwa niaba ya mashirika mbalimbali. Mbili kati ya kodi zinazojumuishwa hapa ni kodi ya michezo ya Kamari na Bahati Nasibu na Ushuru wa Stempu. Ushuru wa Stempu hukusanywa kwa niaba ya Wizara ya Ardhi wakati wa uhamisho wa hisa, au mali.

Kwa kodi ya michezo ya Kamari na Bahati Nasibu, biashara katika sekta ndogo za bahati nasibu, michezo ya kubahatisha, na kuwekeana dau huhifadhi asilimia 20 ya thamani ya ushindi kama kodi na kuikabidhi KRA.

Zaidi ya hayo, asilimia 15 ya jumla ya mapato ya michezo ya kubahatisha kutoka kwa mashirika ya kamari hulipwa kama kodi. Kuweka dau hutozwa asilimia 20 ya ushuru wa kiasi cha pesa zilizowekezwa.

Kodi ya Ongezeko kwa Mtaji (Capital Gains Tax (CGT))

Hii ni kodi inayotokana na faida iliyokusanywa kutokana na uhamisho wa mali ndani ya nchi.

 

Makosa Yanayohusiana na Ushuru Ambayo Yanaweza Kuathiri Biashara Yako Nchini Kenya

Utunzaji wa kumbukumbu Usiofaa

Kushindwa kuweka kumbukumbu sahihi za kifedha hufanya vigumu kufaili kodi yako. Zaidi ya hayo, kama KRA itatambua kuwa una hatia ya hii, wanaweza kutozwa adhabu ya kati KES 10,000 na KES 200,000.

Wajibu Wa Kodi Usio Sahihi

Ili kuepuka hasara na adhabu, wamiliki wa biashara wanashauriwa kujifahamisha na aina zote husika za kodi na pia marekebisho yoyote ya viwango vinavyotumiwa. Kwa mfano, kama mauzo ya kampuni ya kila mwaka ni chini ya KES milioni 5, wanatakiwa kulipa kodi ya mauzo ya asilimia 3 kila baada ya miezi 3. Kwa upande mwingine, kama mauzo ni juu ya KES milioni 5, watahitajika kulipia asilimia 16 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa mauzo.

Kuchanganya Gharama za Matumizi ya Biashara na Binafsi

Sheria inahitaji kampuni kutengenashwa na kutambulishwa tofauti kutokana na wamiliki wake. Katika biashara za mmiliki wa pekee, haya si mahitaji. Hata hivyo, fedha za kibinafsi na za kibiashara zinahitajika kuhifadhiwa tofauti kwani mkaguzi itahitaji uthibitisho kuwa rekodi za mapato na matumizi zilizotolewa zinahusiana na biashara husika.

Muundo Wa Biashara Usio Sahihi

Licha ya kuwa biashara inaweza kuanza kama ushirikiano au mmiliki wa pekee, ni muhimu kutumia huduma ya wataalamu ili kubadilisha muundo huu kisheria wakati ni lazima. Hali hii husaidia kulinda kutokana na adhabu.

Ukwepaji Kodi

Ni kawaida kwa walipa kodi kuhisi kana kwamba serikali inakusanya fedha zaidi kutoka kwao kuliko inavyohitajika. Hatimaye, baadhi yao hutambulisha tu sehemu ya mapato yao. Kama una mpango wa kutumia njia hii, tafadhali usithubutu. Ni kinyume cha sheria! Halikama hii huishia kutozwa kwa kodi maradufu au Shilingi 400,000; yoyote iliyo juu. Pia inaweza kukusababisha kifungo cha miaka 3.

Kuchelewa Kuwasilisha Kodi

Kukaidi kanuni kwa njia hii huwa na adhabu kubwa. Kwa mfano, VAT inapaswa kulipwa kufikia tarehe 20 ya mwezi unaofuata baada ya mauzo. Kushindwa kuwasilisha kodi hii kwa wakati husababisha kutozwa faini ya thamani ya asilimia 5 ya kodi iliyochelewa kuwasilishwa a au shilingi 10,000; yoyote iliyo juu. Utatakiwa kulipa riba ya ziada ya asilimia 2 kwa kila mwezi utakaochelewa kuwasilisha kodi.

Kukosa Kusajili Kama Mlipa Kodi

Baadhi ya biashara hupenda kusalia kama mifumo isiyo rasmi na hivyo kuepuka kusajili biashara hizo na nambari ya utambulisho (PIN) zinazohitajika kwa ajili ya malipo ya kodi nchini Kenya. Mbali na kupokezwa adhabu, hatua hiyo huwa yenye mipaka kwa ukuaji wa biashara yako kwa vile huwezi kupokea mikopo au huduma nyinginezo za manufaa.

Hitimisho

Sehemu mojawapo ya kuwa raia mzalendo ni kulipa ushuru kwa kuwajibika. Kodi iliyokusanywa itasaidia serikali ya Kenya kuendeleza miradi ambayo itasaidia kuendeleza uchumi wa nchi na hali ya maisha ya wananchi. Ili kuwa salama kisheria, ni muhimu kuelewa aina zote zilizopo za kodi nchini Kenya. Pia, ni muhimu kujifahamisha na adhabu zinazohusiana na makosa ya ushuru.