Sawia na maeneo mengine ndani ya Afrika, jumuiya ya Afrika Mashariki imeshuhudia mapinduzi ya kifedha kupitia simu za mikononi. Ama kweli, kwa sasa akaunti za kifedha kupitia simu za mikononi katika eneo hili zimezidi zile (akaunti) za benki ya kawaida. Kuongezeka kwa hali hii ni kutokana na ongezeko la matumizi ya simu za mkononi, kuimarishwa kwa mtandao hata katika maeneo ambayo benki hazipatikani, na urahisi wa kupata huduma mbalimbali za fedha popote ulipo.

Mojawapo ya huduma maarufu ni mikopo ya matandaoni na ya simu. Wenyeji wa Afrika Mashariki wanaweza kupata mikopo kwa haraka bila ya kuwa na wasiwasi kuhusu dhamana au kuhitaji kujaza karatasi. Huku Afrika Mashariki ikiwa imejumuisha mataifa ya ulimwengu wa tatu, wakopeshaji wengi wa kidijitali hutazamwa na wengi kama wakombozi katika wakati wa mahitaji. Wanatoa fedha za ziada zinazohitajika na watu ambao wanaishi kutokana na mishahara yao tu bila vyanzo vinginevyo vya malipo. Baadhi ya mifano katika makala hay ni miongoni mwa taasisi zinazotoa mikopo ya mitandaoni na simu katika Afrika Mashariki.

 

M-Shwari (Kenya)

Hii ni mikopo ya mkononi ambayo ilijitokeza kwa njia ya ushirikiano kati ya Safaricom na Commercial Bank of Africa (CBA). Mbali na muundo wake wa amana, M-Shwari inatoa mikopo ya kati ya shilingi 100 na 50,000 kwa watumiaji wa M-Pesa. Kiwango cha juu cha mikopo kinategemea kiwango cha udeni wa mtu binafsi, na hutozwa riba ya asilimia 7.5. Ni moja ya mfumo maarufu wa mikopo ya mitandaoni nchini. Takriban asilimia 30 ya Wakenya ambao wanamiliki simu za mkononi wamewahi kukopa fedha kutoka mfumo huu na CBA imeidhinisha zaidi ya mikopo 50,000 kila siku.

 

Jinsi ya Kuomba mMkopo wa M-Shwari

 • Nenda kwenye menyu ya M-Pesa kwenye simu yako na uchague Mikopo na Akiba
 • Chagua M-Shwari na kisha Mikopo
 • Omba mkopo kwa kuingiza kiasi unachotaka kabla ya kuweka PIN yako ya M-Pesa
 • Fedha hizo zitatumwa moja kwa moja kwenye akaunti yako ya M-Pesa

Tala (Kenya)

Mikopo ya mkononi ya Tala, ambayo awali ilikuwa inajulikana kama Mkopo Rahisi, ilianzishwa katika soko la Kenya mwaka wa 2014. Ina misingi yake huko Santa Monica na inakisiwa kuwa na thamani ya dola milioni 700. Hutoa mikopo ya kati ya dola 10 na dola 500. Hadi sasa, imetoa zaidi ya dola bilioni 1 kwa wateja wake ambao ni zaidi ya milioni waliomo nchini Kenya na masoko mengine yanayojitokeza kama vile Tanzania, Ufilipino, India, na Mexico. Wafanyakazi wake 500 ni uthibitisho wa ushirikishwaji wa programu hii kwenye orodha ya wakopeshaji mkopo kupitia simu, katika Afrika Mashariki.

One of the online loans in East Africa

Programu ya mkopo ya Tala.

Jinsi ya Kuomba Mkopo Kutoka Tala

 • Pakua programu ya Tala kutoka Google Play Store
 • Sajili akaunti. Kwa kufanya hivyo, utahitaji akaunti ya M-Pesa na pia nambari ya pasipoti au kitambulisho cha kitaifa.
 • Nenda kwenye “Apply Now” na ujibu maswali yaliyowasilishwa
 • Chagua kipindi cha malipo ambayo yanakufaa
 • Bonyeza “Send My Loan”. Fedha zitatumwa kwa akaunti yako ya M-Pesa papo hapo.

Saida (Tanzania)

Mbali na programu za mikopo kama vile Branch na Tala ambazo huhudumu katika nchi zaidi ya moja katika Afrika Mashariki, Saida ni moja ya mfumo mzuri wa wakopeshaji wa kidijitali nchini Tanzania. Ina zaidi ya asilimia 7 ya soko. Tofauti na mipangilio mingine inayopatikana katika soko, mtu anatakiwa kuwa amehifadhi kiasi kikubwa cha fedha kabla ya kuweza kupokea mkopo.

Pindi tu baada ya mkopo huu wa mtandaoni kuidhinishwa, utapokea fedha ndani ya saa moja. Vile vile, utapokea maelezo iwapo maombi ya mkopo wako yatakataliwa. Mojawapo ya hasara yake ni kwamba riba kwa mkopo hutofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine kulingana na alama yako ya kimikopo. Viwango vya riba ni kati ya asilimia 7.5 na 10. Unaweza kupokea kati ya TZS 13,500 hadi Shilingi milioni 2.25. Kulingana na kiasi kilichotolewa, una muda wa siku 30 hadi 60 kulipa mkopo huo.

online loans in East Africa

Programu ya mkopo ya Saida.

Jinsi ya Kuomba Mkopo Kutoka Saida

 • Pakua program ya Saida kutoka Google Playstore
 • Tumia nambari yako ya simu kama njia ya mwaliko. Hatua hii inaweza kuchukua kati ya 3 na 7 siku kukamilika
 • Fungua akaunti ya Saida na ujibu maswali yaliyowasilishwa.
 • Saida itaangalia matumizi yako ya simu kwa ajili ya kumbukumbu ya huduma ya simu ya fedha, data, SMS na kupiga simu. Kulingana na taarifa hii, utafahamishwa kuhusu kiasi cha fedha ambacho unaweza kupata
 • Kiasi cha mkopo kilichoidhinishwa kitatumwa mara moja kwenye akaunti yako ya pesa ya simu. Vilevile utatumiwa maelezo ya kina kuhusu jinsi ya kulipia mkopo huu.

MoKash (Uganda)

MoKash ni bidhaa ya mkononi ambayo inawaruhusu wanachama wake kuhifadhi na kupata mikopo. Tangu kuanzishwa kwa mpango huu mwaka wa 2016, wateja wake wamekuwa wakiongezeka kwa kasi. Kila mkopo unaoidhinishwa hutozwa ada ya mara moja tu ya asilimia 9. Ili uweze kufuzu kwa ajili ya mkopo kwenye mfumo huu, akaunti yako ya pesa ya MTN ya inastahili kuwa hai kwa angalau miezi 6 iliyopita. Zaidi ya hayo, unapaswa kuwa mtumiaji wa MoKash ikiwa ni pamoja na kuhifadhi kiasi kikubwa katika akaunti yako.

 

Jinsi ya Kuomba Mkopo kutoka MoKash

 • Bonyeza 1655# kuanzisha MoKash
 • Nenda kwa ‘Savings and Loans’ na kisha uchague ‘Loans’
 • Nenda kwa ‘Request a Loan’
 • Weka kiasi cha fedha unachotaka kukopa
 • Weka nambari yao ya siri
 • Utapata ujumbe wa uthibitisho kuonyesha kuwa fedha zimetumwa kwa akaunti yako

BK Quick (Rwanda)

Huu ni mfumo wa akiba na mikopo na ulianzishwa na Benki ya Kigali. Ilianzishwa kwa nia ya kutoa jukwaa rahisi kwa wateja wake kufikia baadhi ya huduma za benki hiyo. Mtu anaweza kupata hadi RWF milioni 1 na kurejesha kwa muda wa miezi 1 hadi 12. Kila mkopo wa mkononi hutozwa riba ya asilimia 4. Mkopo uliotolewa hutumwa kwa akaunti ya BK ya mteja. Hakuna ada zinazotozwa kwa ajili ya uhamisho wa fedha kati ya BK Quick na akaunti za BK.

online mobile loans east africa

Mikop ya BK Quick nchini Rwanda.

Jinsi ya Kutuma Maombi ya Mkopo wa BK Quick

 • Sajili namba yako ya simu kwa huduma ya BK MobiServe
 • Piga *334*
 • Nenda kwa ’10 -BK Quick ‘
 • Fuata maagizo na ukubali sheria na masharti yaliyotolewa
 • Fedha zitatumwa mara moja kwenye akaunti yako ya BK

Hitimisho

Kampeni inayoendelezwa kwa ajili ya ujumuishaji wa kifedha katika Afrika Mashariki, pamoja na kuongezeka kwa simu za mkononi na kuimarishwa kwa mtandao, imeunda msingi imara kwa ajili ya ukuaji wa urahisi wa huduma za pesa mkononi. Mikopo ya mtandaoni na simu ni mojawapo ya mienendo ya kifedha wa katika eneo hili. Kuna taasisi mbalimbali zinazotoa fedha kwa wateja papo hapo kwa kiwango cha chini cha riba.