Ajira Zenye Malipo Bora na Malipo Duni Nchini Kenya

Tafsiri:
en_US

Data rasmi kutoka kwa Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Kenya (KNBS) zinaonyesha kuwa idadi ya Wakenya wanaopata chini ya shilingi 30,000 kwa mwezi imeongezeka kwa kiasi kikubwa. Idadi hii imeongezeka kutoka 154,945 (14%) hadi 1,279,982. Ukuaji huu unaashiria asilimia 46.3 ya jumla ya wafanyakazi 2,765,159 wanaolipwa mishahara. Licha ya kupanda kwa gharama za maisha, wengi wa wafanyakazi, takribani asilimia 69, hupokea mapato ya kila mwezi ya chini ya shilingi 30,000 katika sekta za kibinafsi.

best and worst jobs kenya
Shamba la majani chai nchini Kenya. Kilimo huchangia asilimia 34.2 ya Pato la Taifa, lakini ni mojawapo ya sekta ambayo wafanyakazi wake hupata malipo duni.

Ajira Zenye Malipo Bora

Sekta ya fedha na ya mashirika ya kimataifa yasiyo ya kiserikali hulipa mishahara ya ya juu kwa ajira rasmi nchini. Kwa mujibu wa takwimu kutoka Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Kenya (KNBS), mmoja kati ya tano ya wafanyakazi katika sekta hizi mbili huchuma pato la zaidi ya shilingi 100,000 kila mwezi. Wengi wa wale wanaopokea mishahara ya juu zaidi hutoka katika sekta hizi mbili.

1. Mashirika ya Kimataifa Yasiyo ya Kiserikali

Data zilionyesha kuwa mashirika haya yamewajiri jumla ya wafanyakazi 1,345, na 270 kati yao hupokea zaidi ya 100,000 kila mwezi. Watu wanaotafuta ajira au wale ambao wanahitaji kufanya mabadiliko ya ajira huyakimbilia mashirika hayo. Wakati mashirika haya hayana mfanyakazi anayepata chini ya shilingi 20,000 kwa mwezi, asilimia 60 ya wale wa sekta ya kilimo kupokea chini ya shilingi 25,000.

Je, kwa nini mashirika hayo hulipa vizuri? Hii ni kwa sababu wao hupokea ufadhili mkubwa, na wafanyakazi wao ni wataalamu wenye ujuzi. Wataalamu katika sekta hii ni pamoja na wakurugenzi wakuu, maafisa wa programu, na washauri. Wataalamu hawa wanawakilishwa na wafanyakazi katika mashirika ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa.

2. Sekta ya Fedha

Sekta ya fedha ni ya pili kwa kuwalipa wafanyakazi wake vizuri. Data kutoka KNBS inaonyesha kwamba wafanyakazi 11,598 juu ya wafanyakazi wake 75,621 hulipwa zaidi ya shilingi 100,000. Hakuna mfanyakazi katika sekta hii anayepokea chini ya shilingi 15,000 kwa mwezi. Sekta ya fedha, ambayo ni pamoja na kampuni za bima, benki na kampuni za uwekezaji, daima imelenga kupunguza majukumu ya kawaida kama vile kazi za ukarani na kuzipendelea ajira za kimkakati zinazoongozwa na wataalamu wa kulipwa.

Ili kupunguza gharama na kuwafikia wateja zaidi, benki na mashirika ya bima yanaajiri mameneja wenye ufahamu zaidi wa kiteknolojia. Wataalamu ambao hulipwa vizuri zaidi katika taasisi za kifedha ni pamoja na wachambuzi, maafisa wa uwekezaji, mameneja wa matawi, wakuu wa mashirika na wasimamizi waandamizi.

3. Sekta ya Sanaa na Burudani

best and worst jobs in kenya
Sauti Sol ni bendi maarufu nchini Kenya na mojawapo wa wasanii wanaolipwa juu sana.

Sekta hii ni ya tatu kwani 550 wa wafanyakazi wake 7,243 hupokea mshahara mkubwa kila mwezi. Mfanyakazi wa chini sana analipwa shilingi 10,000 kwa mwezi. Wataalamu katika sekta hii ni pamoja na waandaalizi wa matukio, wabunifu wa matangazo, mameneja, wazalishaji wa filamu na vipindi vya televisheni.

Ajira Zenye Malipo Duni

Data ya KNBS pia inaonyesha ajira zinazotoa malipo duni. Sekta katika kikundi hiki zinajumuisha uchimbuaji wa madini, uzalishaji viwandani, kilimo na ajira za majumbani. Sekta ya uchukuzi ilikuwa na idadi kubwa zaidi ya watu wenye pato la juu, takribani 1,578, ambao walikuwa asilimia 1.74 ya jumla ya wafanyakazi 90,647.

1. Sekta ya Kilimo

Hii ni mojawapo ya sekta tanzu za uchumi. Sekta hii inawakilisha aslimia 34.2 ya pato la taifa, ilhali ni moja ya sekta ambapo wafanyakazi hawalipwi vyema. Ina idadi ndogo sana ya wafanyakazi wanaopata zaidi ya shilingi 100,000 kwa mwezi. Wafanyakazi 2,931 tu ndio wapo miongoni mwa wanaopokea mapato makubwa. Hii ni asilimia 12 tu ya jumla ya ajira milioni 2.76 rasmi nchini Kenya. Asilimia 60 ya wafanyakazi wa sekta ya kilimo hupata pato la chini ya shilingi 25,000 kwa mwezi. Takwimu zinaonyesha kuwa wafanyakazi wenye ujuzi duni huishia kufanya kazi zaidi mashambani.

2. Sekta ya Elimu

best and worst jobs in kenya
Mwalimu akiwana watoto wa shule nchini Kenya.

Hii pia ni sekta nyingine kubwa ya uchumi. Sekta ya elimu ina idadi kubwa ya wafanyakazi wanaolipwa chini ya shilingi 30,000 kwa mwezi (21.4% ya wafanyakazi). Sekta hii pia ina idadi kubwa ya wafanyakazi wanaopata juu shilingi 100,000 (watu 17,808). Wao ni pamoja na watawala wa shule, wahadhiri na walimu wa shule za sekondari.

3. Sekta ya Uchimbaji Madini

Sekta hii ina wafanyakazi katika makundi tofauti ya mapato. Wafanyakazi hulipwa baina ya shilingi 0 hadi shilingi 99,999 kwa mwezi. Base Titanium katika mji wa Kwale na Tata Chemicals katika eneo la Magadi ni miongoni mwa kampuni muhimu za madini nchini Kenya, ila wafanyakazi wao wa juu wanalipwa moja kwa moja kwa ofisi zao kuu.

4. Ajira za Majumbani

Wafanyakazi wengi wa nyumbani kama vile wapishi, walinzi wa usalama na wakulima wa bustani hupata chini ya mshahara wa kima cha chini kuanzia shilingi 13,000 hadi shilingi 15,000 kwa mwezi. Licha ya serikali kuweka mshahara wa kima cha chini, ni familia tajiri tu ndizo huzingatia viwango hivi. Takwimu za KNBS zinaonyesha kwamba mapato ya kila mwezi hapa huanzia shilingi 10,000 hadi shilingi 99,999.

5. Sekta ya Uzalishaji Viwandani

Viwanda ni sekta tanzu ya pili baada ya kilimo, na imewaajiri watu 307,592. Kutokana na idadi hii ya wafanyakazi, ni wafanyakazi 6,117 tu (1.9%) waliopo kwenye kitengo cha mapato ya juu. Data rasmi inaonyesha kwamba wafanyakazi 131,557 wana mshahara wa kila mwezi wa chini ya shilingi 30,000.

Hitimisho

Habari hii inaonyesha wazi kuongezeka kwa suala la kukosekana kwa usawa wa mapato nchini Kenya. Ajira zenye mishahara bora ni chache na ni zipo tu katika miji mikubwa kama Kisumu, Mombasa na baadhi ya sekta za huduma jijini Nairobi. Asilimia 2.89 tu ya wafanyakazi katika sekta rasmi hulipwa zaidi kila mwezi huku asilimia 74.58 hulipwa chini ya shilingi 50,000. Hii inaashiria kuongezeka kwa pengo baina ya matajiri na maskini. Ukiwa na mapato ya chini ya shilingi 30,000 ni vigumu kujimudu hasa kwa wale wanaoishi katika maeneo ya mijini. Kutokana na sababu hiyo, watu huwa na hali duni ya maisha na siku zote huishia kutafuta mapato ya ziada.