Vitega Uchumi Vilipavyo Malipo Kwa Kila Mwezi Nchini Kenya

Tafsiri:
en_US

Katika uchumi huu wenye changamoto nchini Kenya, watu wanaangalia njia zitakazowawezesha kupata fedha. Njia nzuri zaidi ni kuwekeza fedha kidogo uliyo nayo ili kuweza kuzalisha mifereji mingi ya fedha. Hebu tuangalie vitega uchumi vilipavyo kila mwisho wa mwezi.

investment montly income kenya

Mfuko Kwa Ajili Ya Soko la Fedha

Hizi ni aina mbili za fedha za maridhiano. Ni fedha zenye kiasi kidogo cha hatari ambazo huwekezwa kwa riba ya hali ya kiwango cha hali ya juu, akaunti za muda mrefu na karibu na fedha taslimu kwenye soko la fedha la Kenya. Ni vizuri kwa wawekezaji wanaotafuta sehemu nzuri ya kuhifadhi fedha zao. Faida inajumuisha riba inayopatikana kila mwezi.

Kukuza mapato yako, inashauriwa kwamba riba iwekezwe tena kwenye soko la fedha. Riba inawekwa kwenye akaunti ya benki ya mwekezaji kwa wawekezaji watakao mtitiriko sawia wa fedha. Vima vya riba, hubadilika badilika kutokana na mienendo ya masoko.

Kwa mfano, kundi la CIC nchini Kenya linazingatia usalama kwa wateja wake na linatoa riba nono kwa wawekezaji. Kiwango cha chini kwa uwekezaji ni Shilingi za Kenya 5000 na nyongeza ya kiasi cha Shilingi za Kenya 1000.

Mfuko wa soko la fedha hautozi gharama za awali. Kuna mambo kadhaa ya kufikiria wakati wa kufungua akaunti ya soko la fedha nchini Kenya. Viwango vya riba, kiwango/kiasi kitolewacho, uwezo na hasara, gharama na masharti ya utoaji.

Mfruko wa Maridhiano (Mutual Funds)

Mfuko wa maridhiano unajumuisha vitega uchumi kutoka kundi la watu na mashirika ili kufanya uwekezaji jumuisho. Makundi haya yanashea faida na hasara za fedha zao. Meneja wa fedha aliyeidhishwa anasimamia fedha hizo. Anafanya chaguzi zote za uwekezaji kwa niaba ya wawekezaji. Mfuko wa maridhiano una riba tofauti tofauti kwenye faida.

Yakupasa pia kuzingatia kwamba mfuko wa maridhiano una hatari. Lakini kama mwekezaji, lazima uwe tayari kupokea hasara. Kuna mifuko kadhaa ya fedha inayofanya vizuri sana nchini Kenya kama Britam Unit Trust, Equity Bank, Old Mutual Kenya na Cytonn Investments.

Mali Isiyohamishika

investment kenya
Mali isiyohamishika nchini Kenya.

Huku kukiwa na kuongezeka kwa idadi ya Wakenya, mali isiyohamishika ni uwekezaji mzuri sana. Hata hivyo, leo hii, kumiliki jengo au eneo, sio rahisi. Hiki kisiwe kikwazo. Muamana wa uwekezaji kwenye mali isiyohamishika (REIT) kama ulivyo mfuko wa maridhiano ni njia sahihi ya kumiliki jengo au eneo la biashara. Faida za uwekezaji kwenye muamana wa uwekezaji kwenye mali zisizohamishika pamoja na kumiliki mali hiyo mara moja, ni kwamba ni rahisi kununua na kuuza hisa. REIT ina kipato kikubwa, ununuzi wa hisa za REIT unahusisha ununuzi wa majengo mengi na sio jengo au eneo moja tu. Pia mameneja wazoefu sana wanashikilia aina hii ya uwekezaji.

Uwekezaji Kwenya Nyumba Za Kupangisha

Kupangisha nyumba kwaweza kuwa uwekezaji mzuri sana iwapo utakuwa na nia ya kumiliki nyumba au jengo lako mwenyewe. Kwanza, utachagua jengo, eneo au nyumba sahihi, inunue au ifanye kitega uchumi, itunze na kisha anza kuipangisha kwa wapangaji. Ununuzi makini huweza kukuinua kifedha. Kwa udhibiti mkubwa na kujitoa sana, utapata fedha nyingi na kuwa na mtiririko mkubwa sana wa fedha kila mwisho wa mwezi.

Wekeza Kwenye Utalii

investment for monthly income kenya
Kenya inajulikana kwa vivutio vya kitalii.

Utalii nchini Kenya ni chanzo kikuu cha pili cha mapato yote ya fedha za kigeni. Fursa zinapatikana kuanzia kujishughulisha na maandalizi ya safari na malazi kwa watalii. Kenya ina mandhari za kuvutia. Changamkia fursa hii ili ujipatia fedha. Waweza kuanzia kwa kuwalenga watalii wa ndani. Andaa safari za kitalii kwenye maeneo mazuri. Wahitajika kuzingatia viwango vya hali ya juu vya kada hiyo na ukarimu. Uwe na mpango mwema na kuwa tayari kujipatia fedha.

Hati za Amana

Benki huzitoa kwa watu binafsi wanaotaka kuwekeza kwa muda maalum na kwa riba zenye kima tofauti tofauti. Ni miongoni mwa akaunti za amana zinazotolewa na mabenki na vyama ya kukopa na kuweka zinazofanya vizuri sana. Hati za amana zaweza kukupatia nafasi ya kujipatia kipato kikubwa cha fedha kuliko hata akaunti ya kawaida. Kwa kuwa na ngazi za hati za amana, waweza kubashiri ni mara ngapi utapenda kutoa pesa zako. Wawza pia kuamua ni kwa muda gani utapenda kuwekeza.

Uwekeji Sekta ya Bidhaa za Rejareja

Sekta hii imo mikononi mwa wachache, na kwa maana hiyo ni muda muafaka kukabiliana nayo. Ukuaji mkubwa wa idadi ya watu unatokea na wawekezaji wanahitaji kuchukua fursa hiyo. Uwekezaji kwa njia ya mtandao nchini Kenya kama vile maeneo ya manunuzi mitandaoni, maeneo ya kulinganisha bei, maeneo ya kujipatia mikopo na maeneo ya kuletewa bidhaa kwa njia ya mtandao, ni maeneo ambayo waweza kuwekeza. Unachohitaji ni kuwa na mkakati na waweza kuwa na uhakika wa kujipatia kipato kizuri kila mwezi.

Wekeza Kwenye Kilimo

investment kenya
Shamba la chai nchini Kenya.

Asilimia 70 ya biashara ya mauzo ya nje ya Kenya, imejikita kwenye kilimo. Hata iweje, watu ni lazima wale. Chakula ni hitaji muhimu sana na iwapo sekta ya kilimo iaendelezwa kitaalamu, wawekezaji watapata faida. Kipindi cha ukame, chakula kinapanda bei na walioko kwenye sekta hiyo wananufaika sana. Waweza hata kuanza na mashine ya kusaga na kuuza unga nchini Kenya ambako ‘ugali’ ndicho chakula kikuu. Uwe na uhakika wa kujipatia kipato kizuri kila mwezi.

Anzisha Biashara Yako

Kuanzisha biashara yako pasi shaka yoyote ndiyo njia kuu zaidi ya kuwekeza ndani ya nafsi yako. Kwa kufanya hivyo, unakuwa bosi wewe mwenyewe na waweza ukatumia chochote ulichonacho ulipo: elimu yako, uzoefu wako wa kazi na vichocheo vingine kwa ajili ya kuanzisha biashara ya maana. Una uhakika wa kujipatia kipato cha kila mwezi kushinda endapo unakuwa umeajiriwa. Unapaswa kujua una uwezo katika mambo yapi na fursa zikuzungukazo. Ukifanya hivyo, hakutakuwa na cha kukuzuia.

Hitimisho

Kenya inafursa nyingi sana za uwekezaji. Masoko mengi yatafunguka kadri serikali inavyoendelea kutengeneza miundo mbinu. Unahitaji jicho la fursa, akili pevu na dhamira ya kufanikiwa.