Makampuni Makubwa ya Kuwekeza (Invest)

Bara la Afrika ni la pili kwa ukubwa baada ya Bara la Asia, kwa ukubwa na kwa wingi wa watu. Kwa miaka kadhaa, bara hili limekuwa likihusisishwa na umaskini, utawala mbaya na miundo mbinu dhaifu. Hata hivyo, kipindi cha miongo miwili iliyopita, bara hili limejipanga upya lenyewe kama mpaka ufuatao kwenye masuala ya kiuchumi duniani.

Kwa kuzingatia sababu kwamba Afrika imevutia umakini wa wawekezaji mbali mbali, makala hii itayapambanua makampuni saba bora yafaayo kwa uwekezaji barani Afrika.

investment in africa

Uchumi wa Afrika

  • Hivi karibuni, Afrika itakuwa eneo huru kubwa zaidi la biashara duniani.
  • Bara hili lina uwiano mkubwa zaidi duniani wa wajasiriamali, japo wengi wao, bado wako kwenye sekta zenye tija ndogo.
  • Ukanda wa Afrika, kusini mwa bara la Sahara, ndilo eneo ‘changa’ zaidi duniani hivi leo, likiwa na zaidi ya asilimia sitini ya watu walio na umri chini ya miaka ishirini na tano.

Je, Afrika Ni Eneo Zuri Kwa Uwekezaji?

Wawekezaji ambao wametupia mkazo zaidi kwa yanayojiri barani Afrika, watakubali kuwa Afrika inavuka kutoka eneo lilihusishwa na mapungufu kuelekea kuwa eneo lenye fursa mbalimbali. Huu ni muda muafaka kuitambua kampuni nzuri ya kuwekeza kwa sababu zifuatazo:

  • Ina idadi kubwa ya wateja wenye uwezo. Afrika ina zaidi ya watu bilioni 1.7, idadi ambayo inatarajiwa kufikia bilioni moja nukta saba ifikapo mwaka 2030. Watu hawa binafsi ni wateja wenye faida kwenye sekta zinazokua za mawasiliano, matumizi ya bidhaa, ukarimu, ujenzi wa majumba, mabenki, afya, elimu na uchukuzi.
  • Uwepo wa wafanyakazi wasio na gharama, wasio na ujuzi, wenye ujuzi kidogo na wenye ujuzi kamili. Nchi za Afrika kwa kiasi, zina ujira mdogo wa malipo kwa saa. Kwa mfano, kima nchini Nigeria, Moroko na Msumbiji kwa sasa ni kwa mtiririko wa dola 0.34, dola 1.62 na dola 0.27. Fursa hii inachagizwa na ukweli kwamba bara hili lina watu vijana zaidi duniani.
  • Matarajio makubwa ya ukuaji. Shirika la Fedha Duniani lilikisia kuwa bara la Afrika litakuwa na matarajio makubwa zaidi ya ukuaji kati ya mwaka 2018 na mwaka 2023. Kufikia mwaka 2030, Afrika itakuwa na zaidi ya robo moja ya wakazi wote duniani wenye umri chini ya miaka 25. Kipengele hiki kinatarajiwa kuongeza uhitaji kwa bidhaa na huduma mbalimbali huku mahitaji kwa kaya yakifikia dola trilioni 2.5 kutoka dola trilioni 1.1 mwaka 2015.
  • Maliasili. Faidaza kuwekeza kwenye nchi za Afrika ni pamoja na kuwepo kwa hazina kubwa ambayo haijaguswa bado ndani ya nchi mbali mbali za Afrika. Utajiri huo ni pamoja na ardhi yenye rutuba, mafuta, umeme unaozalishwa kwa kutumia maji, madini na gesi asilia.

Zipi Ni Hatari Za Kuwekeza Barani Afrika?

  • Masuala ya serikali. Sera ngumu kwenye shughuli za biashara zaweza kuwatisha wawekezaji.
  • Migogoro ya kikanda. Nchi mbalimbali za Afrika zimepambana na migogoro ya ndani kwa miaka mingi. Kuna nyakati, migogoro inachangiwa na mabadiliko ya utawala.
  • Miundo mbinu dhaifu. Baadhi ya nchi za Afrika, bado hazina mitandao ya kuaminika ya barabara, maji na mifumo ya majitaka pamoja na umeme.

Makampuni Yapi Ni Bora Zaidi Kwa Uwekezaji Barani Afrika?

Yapo makambuni mambali mbali ambayo wawekezaji wanaweza kuyafikiria. Makampuni haya yamo nadani ya meneo yakuayo kama vile kilimo, madini, uchukuzi, miundo mbinu, mabenki, afya na elimu. Yanajumuisha:

1. Naspers

investment africa

Naspers ni kampuni kubwa zaidi barani Afrika. Ina soko lenye thamani ya karibu dola za kimarekani bilioni 70. Kampuni inamiliki baadhi ya chapa bora zaidi zinazojulikana Afrika kama Media24, OLX, Takealot, miongoni mwa nyingine nyingi. Kampuni inajulikana sana kwa kampuni yake tanzu ya uwekezaji ambayo imewekeza kwenye makampuni makubwa kama Flipkart, Tencent, Souq na Delivery Hero. Flipkart ilichukuliwa na Walmart kwa dau lenye thamani ya zaidi ya dola milioni 16, wakati Souq ilichukuliwa na Amazon. Tencent imekua mojawapo ya makampuni makubwa zaidi duniani ikiwa na thamani ya soko ya zaidi ya dola bilioni 400 za Kimarekani.

Naspers imeorodheshwa kwenye Soko la hisa la Johannesburg. Miezi michache iliyopita, kampuni hiyo ilianza onesho la barabarani kwa ajili kujiorodhesha kwenye Euronext. Kuna namna mbili za kuwekeza kwenye Naspers. Ya kwanza, waweza kununua hisa moja kwa moja. Hili kwa kiasi ni ngumu miongoni mwa wekezaji wengi wa kigeni kwa sababu ya mchakato mgumu wa ununuzi wa hisa kwenye soko la hisa la Afrika Kusini. Pili, waweza kuwekeza Naspers kwa njia isiyo ya moja kwa moja kwa kununua moja ya mifuko ya kibiashara ya kifedha (ETFs) maarufu Afrika. Baadhi ya mifuko hiyo ni VanEck Vectors Africa Index, IShares na https://www.jse.co.za/trade/derivative-market/equity-derivatives/index-derivatives/equity-index-futures-and-options/msci-south-african-index-futures, miongoni mwa mengine. Kuwekeza kwenye mifuko hii ya kifedha itakuwa ni njia ya kuzimua uwekezaji ndani ya Naspers.

2. MTN

investment africa

MTN Group ni kampuni ya mawasiliano ya Afrika Kusini. Ni kampuni mojawapo kubwa sana barani ikiwa na soko lenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 12 za Kimarekani. Kampuni inafanya shughuli zake kwenye zaidi ya nchi 20 na wateja zaidi ya milioni 300. Imeorodheshwa kwenye soko la hisa la Johannesburg.

Kwenye miaka ya karibuni, Afrika imekuwa moja ya mabara yanayokimbia kwa kasi zaidi duniani. Kuna ongezeko kubwa la watu na idadi ya tabaka la kati inatanuka. Hii imepelekea ongezeko kubwa la mahitaji ya huduma za mawasiliano. Wakati huo huo, hitaji la huduma za uhamishaji wa data na fedha kwa simu kama vile M-Pesa limeongezeka.

Wakati huo huo, MTN hivi karibuni imefikia makubaliano na serkali ya Nigeria juu ya maamuzi ya kutowakatia huduma wateja zaidi ya milioni tano nukta moja. Kampuni imelipa dola bilioni moja nukta tano za kimarekani. Matokeo yake, bei ya hisa zake, imeanza kupanda , kitu ambacho chaweza kuwa ni ingizo zuri. Kama ilivyo kwa Naspers, waweza pia kununua hisa za MTN Group moja kwa moja au kwa kuwekeza katika mojawapo ya mifuko yake mingi ya kibiashara ya kifedha (ETFs).

3. Dangote Group

investment africa

Dangote Group ni kampuni ya Kinigeria inayojivunia kwa kuwa kampuni kubwa zaidi yenye mtandao mpana zaidi wa viwanda Afrika Magharibi na miongoni mwa makampuni makubwa zaidi barani Afrika. Ina kiwango cha mauzo kwa mwaka cha zaidi ya dola bilioni 4 za Kimarekani na mtaji wa soko karibu ya dola bilioni 7 za Kimarekani.

Inafanya kazi kwenye nchi 17 ndani ya bara la Afrika katika sekta zinazokua za mali zisizohamishika na vyakula. Zaidi ya hilo, hivi sasa wanajishughulisha na miradi mikubwa ambayo itaiona kampuni ikiingia kwenye kilimo, kemikali za petroli na pia gesi asilia na mafuta. Kampuni hii kubwa yenye mtandao mpana ina makampuni manne ambayo yote yameorodeshwa kwenye soko la hisa la Nigeria. Hayo ni Dangote Cement Plc, NASCON Allied Industries Plc, Dangote Flour Mills Plc, na Dangote Sugar Refinery Plc.

Sababu kuu ya msingi ya kwanini Dangote Group ni miongoni mwa makampuni bora ya kuwekeza barani Afrika ni ukweli kwamba sughuli zake zimo ndani ya sekta mbili zinazokua barani Afrika. Kwa kuanzia, Afrika ina watu bilioni 1.3. Hesabu hii inatarajiwa kuongezeka kwa kasi kwenye miaka ijayo, huku wachambuzi wakibashiri kuwa itafikia bilioni 1.7 kufikia mwaka 2030. Kwa kujishughulisha na vyakula muhimu ambavyo waafrika wengi wanakula, Dangote Group wamejipanga kimkakati ndani ya uchumi wa bara la Afrika.

Kwa nyongeza, faida ya kampuni kwenye mradi wa mali zisizohamishika inajengwa na dhana mbili: Tabaka la kati la Waafrika linakua kwa haraka na sekta za umma na binafsi zinaendelea kujihusisha na miradi ya maendeleo.

Kama ilivyo kwa makampuni mengine ya Kiafrika kwenye orodha hii, waweza ukawekeza Dangote Group kwa kununua hisa. Waweza pia kutumia njia ya mifuko ya kibiashara ya kifedha (ETFs) kwa kutegemea kwenye ile iliyo imara kama vile Global X MSCI Nigeria au Lotus Halal Equity.

4. SafariCom

investment africa

Safaricom ni Kampuni ya Kikenya ambayo imekua kwa kasi na kuwa moja ya makampuni makubwa ya mawasiliano barani Afrika na kampni yenye faida zaidi ndani ya Afrika Mashariki na Kati. Imeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Nairobi na ina thamani ya soko ya karibu dola bilioni 12 za Kimarekani.

Safaricom inamiliki karibu asilimia 60 ya mawasiliano nchini Kenya. Pamoja na kutoa huduma mbalimbali za mawasiliano kwa watu binafsi na kwa mashirika, Safaricom ni miongoni mwa makampuni yanayoongoza kwenye huduma za kiedha fedha kwa kutumia simu ya mkononi – M Pesa. Kwa hakika, huduma ya fedha kupitia simu ya mkononi imetokea kupendwa kwa eneo kubwa la Afrika. Miamala ifanyikayo kwa kutumia simu za mkononi kwenye ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara ni karibu asilimia 10 ya mapato yote ya ndani ya bara la Afrika.

Kwa hakika, akaunti za fedha kwenye simu za mkononi barani Afrika ni zaidi ya akaunti ya benki. Kwa maana hiyo, kuwekeza kwenye kampuni mojawapo kubwa kwenye sekta hii ni kubashiri kwa uhakika wa kushinda. Mbali ya hilo, Safaricom iko kwenye mchakato wa kutanua huduma zake kwenye nchi nyingine za Afrika kama Ethiopia. Kwa kuzingatia taarifa hizi, Safaricom kwa yakini ni moja ya makampuni bora makubwa ya kuwekeza Barani Afrika. Kuwekeza kwenye kampuni hii kubwa ya Kenya waweza moja kwa moja kununua hisa zake.

5. Standard Bank

investment africa

Standard Bank ni taasisi ya kifedha ya Afrika Kusini. Inashika nafasi ya kwanza Afrika kwenye kwenye makampuni ya ukopeshaji fedha. Inafanya kazi kwenye nchi 19 za Afrika. Kampuni imeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Johannesburg na ina thamani ya karibu dola bilioni 20.

Sekta ya kibenki ni moja ya maeneo yanayokuwa kwa kasi barani Afrika. Hii kwa kiasi kikubwa ni kwa sababu ya idadi inayokuwa kasi ya tabaka la kati, uwekezaji mkubwa kwenye bidhaa na miundo mbinu pamoja na kuongezeka kwa pato la ndani. Kwa ukuaji huu unaotarajiwa kuendelea kukua miaka ijayo, ni sahihi kuwekeza kwenye benki iliyoimarika kama Standard Bank.

Kipengele kingine kinachoifanya taasisi hii ya kifedha kuwa moja ya kampuni bora za kiafrika kuwekeza, ni jitihada zake za hivi karibuni za kuchukua nafasi ya mahusiano ya kibiashara kati ya Afrika na China. Kupitia Makubaliano ya Ushirikiano Baina ya Afrika na China Kwenye Biashara ya Nje (The Africa-China Export Proposition), benki hii imejipanga kama taasisi ya kifedha ikiunganisha wasafirishaji bidhaa wa Afrika na waagizaji bidhaa wa China. Hatua hii inatarajiwa kuongeza thamani ya hisa zake, kitu ambacho kinazidi kuongeza sababu za kuwekeza kwenye benki hii. Pamoja na kununua hisa, mtu anaweza pia kuwekeza kwenye kampuni hii kupitia mifuko ya biashara ya kifedha kama vile IShares, Rydex na Powershares.

6.Jumia Technologies AG

investment africa

Jumia ni kampuni ya Kiafrika ya biashara ya mtandaoni ambayo imekuwa ikijulikana kama Amazon ya Afrika. Ilianzishwa Nigeria na tangu hapo, imepanuka na kuhudumia wateja kwenye mbalimbali ambazo ni pamoja na Misri, Ivory Coast, Kenya na Afrika Kusini. Ina soko lenye mtaji wa karibu dola milioni mia tano za kimarekani.

Kampuni ni moja ya kampuni zinazokua kwa kasi zaidi barani Afrika. Hakika, imekuwa kampuni ya kwanza ya Afrika kuorodheshwa kwenye soko la hisa la New York. Sanjari na mataifa yaliyoendelea kama Marekani na Uingereza, Afrika inakumbatia kwa kasi sana biashara ya mtandaoni. Huku tabaka la kati likiongezeka kila mara, Jumia ni uwekezaji wenye faida.

Dhana hii pia ni mojawapo ya sababu kwanini mradi wake mpya wa ukarimu, unawezekana kupata faida. Kwa nyakati fulani, imekuwa pia ikipata hasara kutokana na gharama walizopata baada ya kuuza hisa kwa umma. Hata hivyo, Kwa mtaji uliopatikana kutoka kwenye mauzo hayo na matarajio makubwa ya ukuaji, Jumia bado ni moja ya kampuni bora sana za uwekezaji.

7. Equity Group Holdings Limited

investment africa

Equity Group Holding Limited ni benki ya nchini Kenya ambayo inatoa huduma nyingi za kifedha. Ni kampuni hodhi ya Benki ya Equity ambayo ndio inaongoza kwa biashara nchini Kenya. Hakika, ndiyo benki kubwa zaidi nchini Kenya kwa vigezo vya idadi ya wateja wake. Imefungua matawi kwenye nchi tano za nyingine za Afrika Mashariki za Rwanda, Sudani ya Kusini, Tanzania, Uganda na Jamhuri Ya Kidemokrasi ya Kongo. Pia ina kampuni tanzu kama vile Finserve na Equity Group Foundation. Ina soko lenye mtaji wa karibu ya dola bilioni 2 na imeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Nairobi.

Benki Ya Equity imejitahidi kutoa huduma kwa eneo kubwa la jumuia ya Afrika Mashariki kwa kujikita kwenye wawekezaji wadogo wadogo walimo ndani ya tabaka la kati. Imeongeza zaidi fursa za biashara kwa kujishirikisha kwenye benki ya kidijitali kutoa huduma za kibenki kwa waishio ughaibuni. Nchini Kenya pekee, faida kutokana na waishio ughaibuni hadi mwezi wa sita mwaka 2019, ilikuwa karibu ya dola milioni 300 za Kimarekani. Hili lilikuwa ongezeko kubwa kutoka miezi ya awali. Hali hii inatarajiwa kuendelea. Vijenzi mkakati hivi vinatarajiwa kuchochea ukuaji zaidi na kisha kuifanya kuwa moja ya kampuni bora Afrika za uwekezaji.

Hitimisho

Kwa miaka kadhaa, Afrika imekuwa ikihusishwa na umaskini, utawala usio na ufanisi na ukosefu wa utawala bora. Wakati hayo yakiwa ni kweli, bara hili lina matarajio makubwa ya ukuaji. Kiuhakika, haya ndiyo makampuni ya Afrika ambayo wawekezaji wanapaswa kufikiria kuwekeza