Jinsi ya Kutuma Pesa Kenya Kwa PayPal

Tafsiri:
en_US

Kenya ni nchi mojawapo yenye uchumi mkubwa barani Afrika. Nchi hiyo inajulikana kwa wanariadha wake, utalii na pia kwenye sekta yake ya fedha. Ripoti ya hivi karibuni imegundua kuwa Wakenya waishio ughaibuni, wametuma nyumbani pesa zaidi ya shilingi za Kenya bilioni mia mbili themanini. Hii ni karibu ya dola za Kimarekani bilioni tatu, na ni zaidi ya fedha zote zilizotumwa kwa nchi zote za Afrika Mashariki.

Hizi ni njia maarufu za utumaji wa pesa kwenda Kenya kutoka ughaibuni.

Katika makala hii, tutaangalia mchakato wa utumaji pesa kwenda Kenya kwa kutumia PayPal.

PayPal ni Nini?

PayPal ni moja ya makampuni makubwa ya teknolojia ya fedha duniani. Hivi tuandikavyo, kampuni hii ina thamani ya zaidi ya dola 120 bilioni za Kimarekani. Makampuni pekee ya teknolojia ya fedha yenye thamani zaidi ya PayPal ni Visa na MasterCard.

PayPal ilianzishwa mwaka 2002 na Peter Thel, Max Levchin, Yu Pan na Elon Musk. Kundi hili mara nyingi hujulikana kama mafia wa PayPal. Thiel aliwekeza kwenye makampuni ya Facebook na Palantir Technologies, Musk alianzisha Tesla na SpaceX wakati Max Levchin alianzisha Slide ambayo iliuzwa kwa kampuni ya Google kwa karibu dola milioni mia mbili. Yu Pan amewekeza kwenye makampuni mengi na alikuwa mwajiriwa wa kwanza wa YouTube.

PayPal iliuzwa kwa eBay kwa zaidi ya dola za Kimarekani bilioni 1,2. Baada ya miaka kadhaa ya ukuaji, kampuni iliuza hisa kwa umma mwaka 2014. Leo kampuni imeshuhudia ukuaji usio wa kawaida na ni miongoni mwa makampuni yanayokua kwa kasi sana duniani.

Jinsi ya Kutuma Pesa Kenya Kwa Kutumia PayPal

Mchakato wa utumaji pesa Kenya kwa kutumia PayPal ni rahisi sana. Kama wewe ni mteja mpya, utahitajika kwanza kujisajili na PayPal. Unachotakiwa ni kuwa na anuani ya barua pepe na kadi ya Credit au Debit. Baada ya kujisajili, utatakiwa kuithibitisha kadi yako. Ili kufanya hivyo, unapaswa kuiunga kadi na akaunti yako na kisha kuithibitisha kwa msimbo wenye tarakimu nne utakaotumiwa na PayPal. Mwishoni, utatakiwa kuthibitisha anuani yako. Unafanya hivyo kwa kupakia bili ya karibuni inayoonesha anuani yako.

Baada ya hapo, unahitajika kuweka fedha kwenye akaunti yako ya PayPal. Njia rahisi zaidi ya kufanya hivyo ni kwa kutumia kadi ya Credit au Debit.

Mwishoni, utahitaji anuani ya barua pepe ya mtumiwa na kumtumia pesa. Njia nzuri ya kutuma ni kumuomba mtumiwa pesa aliyeko Kenya, kutuma ombi la pesa. Hii itakusaidia wewe kutuma kwa anuani iliyo sahihi.

Faida za Kutuma Pesa Kenya Kwa Kutumia PayPal

Kuna faida nyingi uzipatazo kwa kutuma pesa Kenya kwa kutumia PayPal. Baadhi ni hizi:

  • PayPal ni ya haraka. Mtumiwa atapokea pesa papo hapo.

  • PayPal ni salama. PayPal ni miongoni mwa njia salama kabisa za utumaji wa pesa.

  • Paypal ni rahisi kuitumia. Tovuti na mtandao wa kampuni ni rahisi sana kutumia.

Zipi ni Hasara za Kutuma Kesa Kenya Kwa Kutumia PayPal?

Wakati PayPal ni chaguo zuri la kutuma pesa Kenya, ina mapungufu yake. Hasara kubwa za kutumia PayPal kutuma pesa Kenya ni:

  • PayPal ni ghali sana. Inatoza asilimia 2.9 ya pesa yote pamoja na dola 0.30. Kiasi hiki kinaweza kuongezeka.

  • Kiwango cha ubadilishaji fedha hakiaminiki. Mabenki na wengine wenye maamuzi ya kifedha, wana tabia ya kuingilia ubadilishaji wa fedha.

  • Muda mrefu wa kutoa pesa. Inachukua siku tatu kwa pesa kufika kwenye akaunti yako ya benki.

Jinsi ya Kutoa Pesa Kutoka Nchini Kenya Kupitia PayPal

Kiuhalisia, nchini Kenya, zipo njia mbili kuu ambazo mtumiwa pesa aweza kuzitoa pesa kupitia PayPal. Kwanza, wanaweza kuzitoa pesa moja kwa moja kutoka kwenye akaunti zao za benki. Hata hivyo, nchini Kenya, ni benki ya Equity pekee ndiyo yenye uwezo huo. Haiwezekani kutoa pesa kwenye akaunti za benki za Standard Chartered, Ushirika, Familia, na kadhalika.

Kuzitoa pesa kupitia benki ya Equity, kwanza unapaswa kuiunga akaunti yako ya PayPal na akaunti yako ya benki ya Equity. Baada ya hapo, ingia kwenye akaunti yako ya benki ya Equity, chagua akaunti yako ya PayPal na kiasi unachotaka kutoa. Utapokea barua pepe ya uthibitisho baada ya muamala kukamilika. Fedha zinatumia siku tatu kuingia kwenye akaunti yako.

Paypal to Equity Bank
Benki ya Equity na PayPal

Chaguo jingine ni kutoa pesa zako kupitia M-Pesa. Kampuni ya SafariCom imeingia ubia na PayPal na kampuni iitwayo Thunes inayowezesha muamala huu kufanyika. Ili kufanya muamala, inakubidi uiunge nambari yako ya M-Pesa na akaunti yako ya PayPal. Unafanya hivyo kwa kujiandikisha kwa kampuni kwa kutumia kiunganishi hiki. Baada ya kuunganisha akaunti hizo mbili, unaweza kutoa pesa. Mara nyingi pesa huingia kwenye akaunti yako ya M-Pesa sio chini ya siku moja.

Njia Nzuri Mbadala wa PayPal Nchini Kenya

Msimbo kuponi wa WorldRemit

Ofa maalum hadi mwezi wa tatu mwaka 2020. Tuma pesa Kenya kwa kutumia WorldRemit kwa kutumia msimbo 3FREE na hulipii gharama za utumaji kwa miamala yako mitatu ya kwanza. Msimbo kuponi WorldRemit kwa uhamishaji pesa bure.

Kama ilivyosemwa hapo juu, PayPal ni chaguo zuri, lakini ina pia hasara zake. Hivyo waweza kufikiria njia nyingine za haraka na za gharama nafuu kutuma pesa Kenya. Machaguo mengine ni:

  • TransferWise: Hii inatuma pesa kwenda akaunti ya benki iliyoko Kenya au kwa M-Pesa kwa gharama kidogo.

  • WorldRemit: Hii iko sawa tu na TransferWise. Tofauti ni kwamba waweza kuchukua pesa kutoka kwa mawakala wake wengi.

  • Bank Transfer: Hii inawezesha pesa kuhifadhiwa moja kwa moja kwenye akaunti yako ya benki. Inachukua siku moja tu kwa pesa kuwasili.

  • Bitcoin: Waweza kutuma pesa haraka kwa kutumia Bitcoin. Kuna gharama kidogo na mpokeaji pesa nchini Kenya, atazibadilisha mara moja.

Hitimisho

PayPal ni mtandao mkubwa na ni moja ya makampuni makubwa duniani. Kampuni hii inakuwezesha kutuma pesa nchini Kenya na kwenye makampuni mengine ya Afrika. Tahadhari kubwa ni kuizuia kumtumia pesa mtu usiyemjua. Tahadhari nyingine ni kuihakiki anuani ya mtumiwaji mara kwa mara.