Uchumi wa Kenya na Sensa ya Watu na Makazi ya 2019

Kutokana na matokeo ya takwimu ya sensa ya watu na makazi 2019, Kenya ina idadi ya watu 47,546,296. Kati ya hayo, 23,548,056 ni wanaume huku 24,014,716 ni wanawake wanaowakilisha asilimia 50.5 na 1,524 waliorodheshwa kama wenye jinsia mbili. Sensa ya awali ya 2009 ilionyesha kulikuwa na jumla ya Wakenya milioni 37.7 hii ikiwakilisha ukuaji wa 2.2 wa baina ya sensa ya mwaka 2009 na 2019. Kiwango cha ukubwa wa kaya (familia) pia kilipungua kutoka 4.2 mwaka wa 2009 hadi 3.9 mwaka wa 2019.

kenya population and economu
Kenya ni nchi ya kwanza ya Afrika kuwahesabu watu wa jinsia mbili.

Kulingana na ripoti ya Benki ya Dunia, Kenya, inayojulikana kama “Silicon Savannah,” inahitajika kubuni fursa kwa wakazi wake wanaozidi kukua. Kwa kuweka mazingira mazuri ya kutekeleza shughuli, wananchi wanaweza kuzindua kazi na hivyo kuukuza uchumi. Sekta ya Teknolojia Habari na Mawasiliano imekua kwa kiasi kikubwa cha kiwango cha 10.8% kutoka 2016. Kwa sababu hiyo, Kenya inapaswa kuanza kuikumbatia ajira ya kidijitali.

Sensa ya Kenya

  • Sensa ya 2019 ni zoezi la nane la kitaifa tangu nchi kupata uhuru mwaka 1963. Sensa ya kwanza nchini Kenya ilifanyika mwaka 1948, wakati Kenya ikiwa bado koloni la Uingereza.
  • Sensa ya 2009 iliweka kumbukumbu ya idadi ya watu wenye jinsia mbili kwa mara ya kwanza.
  • Kaunti tano zenye idadi kubwa zaidi ya wakazi ni pamoja na mji mkuu wa Nairobi, Kiambu, Nakuru, Kakamega na Bungoma.
  • Kenya ni taifa la kwanza la Afrika ya kutoa matokeo ya sensa yaliyosindikwa kabisa katika kipindi cha mwaka mmoja baada ya kutekelezwa.

Sekta Muhimu Katika Uchumi wa Kenya

kenya census economy
iHub ni mojawapo wa vitovu tanzu nchini Kenya vya kiteknolojia maarufu
Silicon Savannah.

Sekta tanzu kwa uchumi nchini ni kilimo, misitu, madini, uvuvi, uzalishaji wa kiviwanda, utalii, nishati, na huduma za kifedha. Robo ya pili ya Pato la Taifa inaonyesha kuwa uchumi wa Kenya ulikua kwa asilimia 5.9, ambayo ni ishara ya kushuka kutoka asilimia 6.4 mwaka 2018. Kushuka kwa Pato la Taifa kulitokana na kupungua kwa shughuli za kilimo, viwanda na uchukuzi. Kilimo na usambazaji wa nguvu za umeme ulioathirika kutokana na kuchelewa kwa mvua za masika huku sekta ya usafiri ikiathiriwa na ongezeko la bei ya mafuta.

Miongoni mwa sekta ambazo zilifanya vizuri ni pamoja na huduma za makazi na malazi kwa wasafriri, na huduma za chakula, habari na mawasiliano, viwanda vya ujenzi, na biashara za jumla na rejareja. Sekta ya Habari na mawasiliano ilikua kwa asilimia 11.6, malazi na huduma za chakula iliongezeka kwa asilimia 10.6, huku ujenzi ilikua kwa asilimia 7.2. Sekta ya fedha na bima ilisajili kuboreka zaidi kwa kiwango cha asilimia 2.1, ikifuatiwa na sekta ya ujenzi ikijiboresha kwa asilimia 1.8.

Mnamo Septemba 2019, Faharasa ya Bei (Consumer Price Index) ilipungua kutoka 201.78 mwezi wa Agosti hadi 201.57 mwezi wa Septemba, ikiashiria kupungua kwa asilimia 0.11. Kiwango cha mfumuko wa bei mwezi wa Septemba mwaka 2019 kilikuwa asilimia 3.83.

Ruwaza ya 2030

Ruwaza ya 2030 ni mwonozo wa muda mrefu wa maendeleo ya Kenya ulionuiwa kuendeshwa kutoka mwaka wa 2008 hadi 2030. Ruwaza hii inalenga kubadilisha Kenya hadi kuwa kitovu cha viwanda cha kipato cha kati na kuchangia kwa maisha bora kwa wananchi wake kufikia mwaka wa 2030. Maono yaliasisiwa ili kuwezesha Mkakati wa Kukwamua Uchumi pamoja na kuzindua nafasi za ajira.

Nguzo tatu zinayasaidia maono haya; nguzo ya kiuchumi, nguzo ya kijamii, na nguzo ya kisiasa. Nguzo ya kiuchumi inarejelea maendeleo ya kiuchumi nchini na kuhakikishia taifa kuwa pa ukuaji wastani wa uchumi kwa asilimia 10 kila mwaka. Nguzo ya kijamii inalenga kuhakikisha kwamba Wakenya wanaishi katika jamii yenye mshikamano, yenye umoja na usawa wa kijamii na katika mazingira safi. Lengo la nguzo ya kisiasa ni kuutambua mfumo wa kidemokrasia wa kisiasa ambao unazilinda haki za raia wake kulingana na utawala wa kisheria.

Kufanya Biashara Nchini Kenya

Sekta ya kibinafsi imekuwa ikiongoza katika ukuaji wa uchumi wa Kenya tangu miaka ya 2000. Ni kutokana na sababu hii ndipo serikali imepania kutekelezwa kwa ruwaza ya 2030 kwa sekta muhimu za uchumi. Serikali imeelekezea makini katika sekta muhimu za uchumi, viwanda, usalama wa chakula, nyumba za bei nafuu na huduma za afya kwa kile imetambulisha kama Ajenda Nne Kuu.

Wakati wa mkutano wa Biashara Huria wa Bara la Afrika (AfCFTA) mwaka 2018 uliofanyika mjini Kigali, Kenya na nchi nyinginezo 43 zilitia saini makubaliano. Malengo ya mkataba huu ni kuwezesha soko la idadi ya zaidi ya watu bilioni 1.2. Pato la Taifa kutokana na soko hili ni dola trilioni 3.4 na inalenga kuongeza biashara miongoni mwa mataifa ya bara Afrika kwa dola bilioni 34.6 itakayoashiria ongezeko la asilimia 52.3 kufikia mwaka 2022.

Ili kuanzisha kampuni nchini Kenya, hatua za awali zinajumuisha usajili wa jina la kampuni lililopendekezwa kwa msajili wa kampuni. Shughuli hufanyika katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu katika jiji kuu. Pamoja na hilo, unahitaji kuwasilisha mkataba wa chama na makala ya chama kwa msajili wa kampuni. Iwapo ataridhishwa na uliyowasilisha, utakabidhiwa cheti cha usajili.

Hitimisho

Kenya ina uchumi imara unaosaidia uwekezaji katika sekta mbalimbali. Serikali inaweka mikakati anuwai ya kukuza biashara ndogo, hasa kwa kuweka kiwango cha riba kitakachotozwa na benki. Hatua hii ya hivi karibuni inaangazia maslahi yatakayosaidia biashara ndogo ndogo kuweza kupata mikopo. Ruwaza ya 2030 na Ajenda Nne Kuu ni miongoni mwa mipango ya serikali ya kusaidia kuusisimua Uchumi wa Kenya hadi kuwa wa mapato ya kati na hivyo basi kusaidia kuleta mabadiliko kwa maisha ya Wakenya.